Back to Top

Yanga yatoa neno kuhusu sakata la Kabwili

 Wednesday, January 29, 2020   


Uongozi wa klabu ya Yanga umeibuka na kufunguka kuhusu  sakata la tuhuma za upangaji matokeo zilizoibuliwa na mlinda mlango, Ramadhani Kabwili alipokuwa akiituhumu timu ya simba ambapo alidai kuaidiwa gari aina ya IST.

Akizungumzia tulio hilo, Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wao kama klabu walilamikia tukio hilo mnamo Februari 12, 2019  na kocha Mwinyi Zahera, na kwamba alichokifanya Kabwili ni kuelezea historia ya tukio lenyewe lilivyokuwa.

"Kilichofanywa hapa na Kabwili ni kuelezea historia ya tukio hilo kwa uzoefu wake kwenye kucheza mechi kubwa kama ile na umri wake ni mdogo pamoja na changamoto ambazo alikutana nazo", amesema Bumbuli.

"Kwahiyo kwa sababu suala limekuwa hivyo na sisi tumemuita mchezaji wetu tukae naye na atueleze kinagaubaga nini kimetokea, tukusanye ushahidi wote na tuupeleke kwenye vyombo vinavyohusika", ameongeza.

Mtazamo wa wengi unatofautiana kuhusu suala hilo, wapo wanaosema kuwa Kabwili amekosea kulisema suala hilo katika chombo cha habari na badala yake angelipeleka TFF tena mapema zaidi na wapo wanaosema yupo sahihi kwa kuwa masuala nyeti kama hayo hayapaswi kufumbiwa macho katika soka.

0Comments

Post a Comment