Back to Top

Shirika la Ndege la Uingereza lasitisha safari za kutoka London kuelekea China

 Wednesday, January 29, 2020   

Shirika la Ndege la Uingereza limesitisha kwa muda safari za moja kwa moja za kutoka London kuelekea China kutokana na hofu ya maambukizi na kusambaa kwa Virusi cya Corona.

Hadi kufikia sasa zaidi ya watu 100 wameshafariki kutokana na homa inayosababishwa na virusi hivyo. Wengi wa watu walioambukizwa wapo katika mji wa Wuhan ambapo ndipo vilipozuka virusi hivyo.

Idadi ya vifo vya kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona imeongezeka hadi kufikia watu 106 hali ambayo inaleta wasiwasi ulimwenguni kote. Kisa cha kwanza kimeripotiwa nchini Ujerumani. Maelfu ya raia wa kigeni wamekwama katika mji huo wa Wuhan, huku mataifa tajiri ikiwa ni pamoja na Marekani na nchi nyengine zinajiandaa kuwaondoa raia wake kutoka kwenye jiji la Wuhan ambalo ndio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo.

0Comments

Post a Comment