Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuwa mgeni rasmi kongamano la UVCCM Arusha Februari 1 mwaka huu
Wednesday, January 29, 2020
Na Ferdinand Shayo,Arusha
Kongamano kubwa la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Wilaya zote za mkoa wa Arusha na nje ya Mkoa wa Arusha linatarajia kufanyika februari 1 mwaka huu Katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano (AICC) huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James.
Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM na Chipukizi Mkoa wa Arusha Edson Rudovick Ndyemalila amesema hayo akizungumza na Muungwana Blog juu ya kongamano hilo kubwa linalotarajia kufanyika jijini Arusha ambapo vijana zaidi ya 600 watahudhuria.
Edson amesema kuwa kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Vijana ndio nguvu kazi ya taifa na chama na chem Chem ya fikra mpya za maendeleo endelevu" .
Aidha amewakaribisha vijana wote wa mkoa wa Arusha kuhudhuria kongamano hilo linalohamasisha uzalendo,uadilifu na uwajibikaji kwa vijana ili kushiriki katika maendeleo ya taifa.

0Comments
Post a Comment