Back to Top

Idadi ya vifo vitokanavyo na mafuriko vyaongezeka Lindi

 Wednesday, January 29, 2020   

Idadi ya vifo imeongezeka Mkoani Lindi na kufikia Watu kumi kufuatia mafuriko yaliyovikumba baadhi ya Vijiji Mkoani humo, Watu wengi wamepoteza Makazi yao.

Vikosi vya uokoaji vimeokoa zaidi ya Watu 1000 mpaka sasa katika kijiji cha Njinjo pekee ambacho kinaonekana kuathirika zaidi Wilayani Kilwa huku baadhi ya Wananchi wakidai kupotelewa na Ndugu zao.

"Wengine wanasema wamepotelewa na Ndugu lakini hadi tuthibitishe lakini kwa hali ilivyo hatutoshangaa kuona idadi ya vifo imeongezeka, hali ni mbaya sana" - Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa Lindi

0Comments

Post a Comment