Samatta aonyesha uwezo wake, timu yake yatinga fainali
Wednesday, January 29, 2020
MBWANA Samatta, mshambuliaji wa timu ya Aston Villa, amecheza mchezo wake wa kwanza usiku wa wa kuamkia leo mbele ya Leicester City kwenye Kombe la Carabao, Uwanja wa Villa Park na timu yake imetinga hatua ya fainali.
Bao pekee la ushindi la Aston Villa lilifungwa dakika ya 90+3 na Mohamoud Hassan.
Samatta alifunga bao la kwanza kwenye mchezo wake wa leo dakika ya 37 ila mshika kibendera alidai kuwa mtoa pasi alikuwa ameotea.
Dakika ya 64 Samatta alikosa bao la wazi akiwa na mlinda mlango kwa kushindwa kuitumia pasi ya mchezaji mwenzake akiwa ndani ya 18 jambo lililomuuza nyota huyo
Dakika ya 66 Samatta alitolewa nje na nafasi yake ilichukuliwa na Keinan huku Wachezaji wawili wa Aston Villa walionyeshwa kadi ya njano ambao ni Konsa na Luiz.
Aston Villa wametinga Fainali ya michuano hiyo huku wakimsubiri mshindi kati ya Manchester City au Man United na wameitoa Leicester City kwa jumla ya mabao 3-2.


0Comments
Post a Comment