Back to Top
Update: Watu 176 wafariki katika ajali ya ndege Iran Wednesday, January 08, 2020 Imeripotiwa kuwa zaidi ya watu 176 wamefariki dunia kufuatia na ajali ya Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria zaidi ya 170 iliyoanguka Iran. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege namba PS752 hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.

0Comments

Post a Comment