Back to Top

Marufuku kuzuia kusajili watoto darasa la kwanza kwa kukosa vyeti vya kuzaliwa- Jafo

 January 08, 2020 Waziri wa Ofisi ya Tawala Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI), Selemani Jafo amepiga marufuku watoto kuzuiliwa kuandikishwa darasa la kwanza sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa. Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), jijini Dodoma ambapo amesema watoto kupata elimu ni haki yao. "Ni marufuku kuwazuia watoto kusajiliwa kuanza Darasa la kwanza, ila wale ambao hawana vyeti vya kuzaliwa wazazi na RITA ihakikishe ndni ya miezi mtoto anapata cheti cha kuzaliwa."

0Comments

Post a Comment