Back to Top

Wadaiwa sugu NHC kukiona

 Wednesday, January 29, 2020   

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetangaza kuanza kuwachukulia hatua wapangaji ambao ni wadaiwa sugu ikiwamo kuwaondoa kwenye nyumba na kukamata mali zao na kuzinadi

Sambamba na hilo, shirika pia limesema litafanya tathmini ya mikataba iliyoingiwa kati yake na wabia ili kuona kama inafuatwa kwa mujibu wa makubaliano ili kuondoa sintofahamu kati ya pande husika.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulid Banyani, alisema jana akiwa katika ziara kwenye mkoa wa NHC Temeke kukagua miradi ya shirika iliyoingia mkataba na wabia, huku akiwataka wapangaji wote wanaodaiwa kulipa malimbikizo kabla ya kufikiwa na zahama hiyo.

Alisema katika kutekeleza hilo, shirika halitakuwa na huruma na wapangaji ambao wamekuwa hawatekelezi wajibu wao kwa sababu wanalikosesha shirika fedha ambazo zingefanya shughuli za maendeleo.

“Rai yangu kwa wapangaji ni kuhakikisha wapangaji wote wanalipa kodi kwa wakati na kukamilisha malimbikizo ya kodi wanazodaiwa. Baadhi ya wapangaji wanakiuka taratibu za mikataba yao katika kulipa kodi kwani wamekuwa si waaminifu katika kulipa kodi kwani wamekuwa na malimbikizo makubwa jambo ambalo linakiuka mkataba wa upangishaji walioingia na shirika,” alisema.

“Mpangaji wa NHC aliyepanga nyumba ya malazi au eneo la biashara, ana jukumu la kulipa kodi yake kwa wakati kama ambavyo mkataba unamtaka kufanya, lakini baadhi yao wamekuwa wakilimbikiza malipo hayo jambo ambalo ni kinyume cha mkataba waliongia na NHC,” alisisitiza.

Katika kutekeleza hilo, alisema shirika halitamwonea haya mpangaji ambaye ana malimbikizo ya kodi kwa kuwa tayari lilishatoa muda kwa wapangaji ambao wana malimbikizo kufika katika ofisi za NHC kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kuona namna wanavyokamilisha malipo yao ya kodi wanazodaiwa.

Dk. Banyani alitahadharisha kuwa wapangaji wote ambao hawatakamilisha malipo ya kodi wanazodaiwa, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwamo kutangazwa kwenye vyombo vya habari na hatimaye kuwatimua wale watakaoshindwa kulipa.

Katika ukaguzi wa majengo ya ubia yaliyoko katika Mkoa wa Temeke, Dk. Banyani alisema NHC itapita kila jengo ili kuhakikisha taratibu zilizowekwa zinafuatwa na ikiwa umekiukwa, watu hao watafikishwa katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu alisema majengo yote ya ubia yatafanyiwa tathmini upya ili kuona mikataba iliyoingia NHC na wabia hao inafuatwa na kutekelezwa kwa maslahi ya wote bila kuwa na migogoro.

0Comments

Post a Comment