Back to Top

Safaree ajibu mapigo kwa Nicki Minaj baada ya kuchafuliwa vibaya

 Wednesday, January, 29, 2020  

Baada ya Jumanne hii kuwa siku mbaya sana kwa Safaree Samuels baada ya kupakwa tope zito na aliyekuwa mpenzi wake, Nicki Minaj, rapper huyo amejibu mapigo ya tuhuma nzito.

Jumanne hii kupitia kipindi cha Hot 97 kinachoendeshwa na DJ Funkmaster Flex, Nicki alikuwa akimuhudumia kila kitu na kumjali lakini ilifika muda mpenzi wake huyo [Safaree] alikuwa anaiba kadi yake ya benki na kwenda kutoa pesa na kununua wanawake wengine.

Queen huyo wa Cash Money, alifichua siri nyingine ambayo ex wake huyo alikuwa akijinadi kuwa alikuwa akimuandikia ngoma Minaj kipindi chote cha nyuma. 

Baada ya kuchafuliwa huko Safaree aliamua kuhamia kwenye mtandao wa Twitter na kuandika maneno mazito ikiwemo kufichua kuwa Nicki aliwahi kumchoma kisu na kutokwa na damu nyingi mpaka kukaribia kupoteza maisha lakini polisi walipofika rapper huyo alimtetea Nicki kwa kusema alijichoma mwenyewe akitaka kujiua. 

Safaree alimaliza kwa kusema anapoelekea Nicki Minaj sio kuzuri maana haya sio mambo ambayo anastahili kufanya mtu kama yeye kipindi hiki cha kuitangaza album yake kwa kuwa amekuwa akitumia nguvu nyingi sana.

0Comments

Post a Comment