Back to Top

Rais Trump amshambulia Bolton wakati kesi yake ikipamba moto

 Wednesday, January 29, 2020   

Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza mashambulizi kwa mshauri wake wa zamani wa usalama wa taifa Michael Bolton, ambaye kitabu chake kinachosubiriwa kuzinduliwa huenda kikaathiri utetezi wa Trump katika kesi inayomkabili katika baraza la Seneti.

Trump ameandika kwenye Twitter kuwa alimtimua Bolton kwa sababu kama angemsikiliza basi tungekuwa sasa katika Vita Kuu vya Sita vya Dunia.

Amemshambulia akisema kitabu chake kina uwongo mtupu na kuwa masuala yote ya usalama wa taifa huwa ya siri na hayapaswi kutolewa kwa umma.

Wademocrat wanataka Bolton atoe ushahidi katika kesi ya rais inayoendelea kwenye baraza la Seneti, na kumekuwa na dalili zinazoongezeka kuwa maseneta wa kutosha wa Republican huenda wakaunga mkono wito huo.

0Comments

Post a Comment