Back to Top

Necta yatangaza matokeo ya kidato cha nne, wanafunzi bora Kitaifa, shule 10 zilizoongoza Dar hakuna hata moja

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili kwa mwaka 2019.
Image
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema kuwa ufaulu umeongeza kwa asilimia 1.38.
“Kati ya Watahiniwa 422,722 wa kidato cha nne waliofanya mitihani mwaka 2019, 340,914 sawa na asilimia 80.65 wamefaulu, na ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.38” amesema Charles Msonde  Katibu Mtendaji NECTA
Dk Charles Msonde amesema kuwa “Wasichana waliofaulu 175,296 sawa na asilimia 79.46 na wavulana ni 165,618 sawa na asilimia 81.94.”
Orodha ya Shule 10 bora Kitaifa ambazo zimefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne kwa miaka 3 mfululizo.
Image
Orodha ya wanafunzi 10 bora Kitaifa waliofanya vizuri kwenye Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2019.
Image
Orodha ya wanafunzi wakike 10 bora Kitaifa waliofanya vizuri kwenye Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2019.
Image

0Comments

Post a Comment