Back to Top

Mvua zinazoendelea kunyesha zaleta maafa Lindi, Watu wanne wafariki

 Tuesday, January 28, 2020   

Watu wanne wamefariki Dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Lindi huku nyumba nyingi zikisombwa na maji na Barabara kuharibika .

"Watu wawili Wilaya ya Lindi na wawili Wilaya ya Ruangwa wamefariki kwa kusombwa na maji, kule Njinjo, Wilayani Kilwa hali ni mbaya tumechukua Boti kwenda kuokoa" - Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi

"Nawaomba Wananchi hasa wanaotembea kwa miguu na vyombo vya Moto kutotembea usiku kwa kuwa mvua hizi zinapasua sana Barabara" - ZAMBI

0Comments

Post a Comment